• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yachukua hatua za mageuzi ya matibabu na afya ili kuwanufaisha zaidi wananchi

  (GMT+08:00) 2017-07-24 18:37:09

  Katika wiki iliyopita, baada ya kufanya mazungumzo na kampuni za kutengeneza dawa, aina 36 za dawa za magonjwa makubwa ikiwa ni pamoja na saratani zimewekwa kwenye orodha za dawa zilizomo kwenye bima ya matibabu, wakati huo huo wastani wa bei ya dawa hizo utapungua kwa zaidi ya asilimia 40, hali ambayo itachangia kupunguza mzigo wa kifedha kwa wagonjwa. Huu ni mwaka muhimu kwa China kuhimiza mageuzi ya utaratibu wa matibabu na afya, ambapo China itafanya mageuzi na kukamilisha sera za utengenezaji, uuzaji na matumizi ya dawa, na utaratibu wa upatikanaji wa faida kutokana na uuzaji wa dawa katika hospitali ya serikali utaondolewa kabisa.

  Dawa zina uhusiano wa karibu na afya ya wananchi. Tangu hatua za kuhimiza mageuzi ya matibabu zianze kutekelezwa, utaratibu wa kimsingi wa dawa za China umeanzishwa kwa hatua ya mwanzo, hali ambayo imehakikisha utoaji wa dawa, na kupunguza bei za dawa hatua kwa hatua. Lakini bei za juu kupita kiasi zinazoleta faida kubwa ya uuzaji wa dawa ziliwaletea wagonjwa mzigo mkubwa kifedha. Mwanzoni mwa mwaka huu, serikali ya China ilitoa waraka ikisisitiza kuwa, ili kuondoa utaratibu wa upatikanaji wa faida kutokana na uuzaji wa dawa, ni lazima kupunguza mzigo wa gharama kubwa za dawa kwa jamii nzima. Mkurugenzi wa Ofisi ya mageuzi ya matibabu kwenye Baraza la serikali la China ambaye pia ni naibu mkurugenzi wa Kamati ya afya na uzazi wa mpya Bw. Wang Hesheng anasema:

  "Hatua ya kwanza ni kuhimiza hospitali kutumia dawa za kimsingi zilizoidhinishwa na serikali, kuimarisha usimamizi kuhusu matumizi ya dawa, na kuhimiza matumizi ya njia mwafaka ya dawa. Pili, kuondoa utaratibu wa upatikanaji wa faida kutokana na uuzaji wa dawa, kudhibiti kwa makini ongezeko lisilo mwafaka la gharama za dawa. Tatu, kuhimiza kwa nguvu mageuzi kuhusu njia ya ulipaji wa bima ya matibabu."

  Mbali na hayo, China pia itaharakisha hatua za ukaguzi na uthibitishaji wa dawa za aina mpya zinazohitajika na zinazokosekana, ili kuwanufaisha wagonjwa mapema zaidi. Idara ya afya na uzazi wa mpango ya China imeeleza kuwa, itaboresha utaratibu wa utoaji wa matibabu kwa njia ya upashanaji wa habari, ili kutoa huduma rahisi, zenye usalama na ufanisi mkubwa zaidi kwa watu. Naibu mkurugenzi wa Idara ya usimamizi wa mambo ya matibabu kwenye Kamati ya Afya na Uzazi wa Mpango ya China Bi. Jiao Yahui anasema:

  "Tutatumia njia mbalimbali za upashanaji wa habari ili kutoa huduma bora za matunzo, utoaji wa habari, uhasibu wa gharama za matibabu, ili kuboresha hali ya wananchi wakati wa kupewa matibabu na kupunguza muda wa kusubiri hospitali."

  Licha ya hayo, China itaonesha vya kutosha kazi ya matibabu na dawa za jadi za kichina katika kuhakikisha afya ya wananchi, pia kuimarisha ujenzi wa kituo cha utoaji wa huduma za afya kwenye sehemu za mashina nchini, kukamilisha utaratibu wa utoaji wa huduma za afya, na kuhimiza kuwepo kwa uwiano kwa utoaji wa huduma za afya kwa raia kote nchini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako