• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Idara ya Utalii ya Kenya yajitangaza kiutalii nchini China

    (GMT+08:00) 2017-07-24 18:59:05

    Shughuli ya kutangaza utalii wa Kenya iliyoandaliwa na idara ya utalii ya Kenya imefanyika katika ubalozi wa Kenya nchini China.

    Kwenye shughuli hiyo, mpango wa utoaji wa mafunzo kwa "Wataalamu wa Utalii wa Kenya" kwenye mtandao wa Internet umezinduliwa rasmi hapa China. Wakati huohuo, mpango wa shughuli mfululizo za kuhimiza utalii wa China zinazolenga soko la China pia umetolewa, ili kuwavutia watalii wengi zaidi wa China kutalii nchini Kenya na kusukuma mbele maendeleo ya sekta ya utalii ya Kenya.

    Afisa ubalozi anayeshughulikia mambo ya biashara Bw. Vincent Omuse amesema, idadi ya watalii wa China wanaoenda Kenya inaendelea kuongezeka tangu mwaka 2004. Idadi hiyo katika mwezi Januari hadi Julai mwaka jana iliongezeka kwa asilimia 68.9 ikilinganishwa na mwaka 2015. Bw. Omuse amesema, serikali ya Kenya imeweka lengo kubwa zaidi katika soko la utalii la China.

    "Serikali ya Kenya imetambua uwezo mkubwa wa China ikiwa soko kubwa kwa utalii wa Kenya. Hivyo serikali ya Kenya imeweka lengo la muda mfupi na wa wastani linalolenga kuongeza idadi ya watalii wa China kutoka elfu 40 hadi laki 1 kila mwaka."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako