• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Israel yawakamata wafuasi 25 wa kundi la Hamas

    (GMT+08:00) 2017-07-24 19:26:19

    Kamati ya usalama wa taifa ya Israel na kikosi cha ulinzi cha Israel wamewakamata wafuasi 25 wa kundi la Hamas katika ukingo wa magharibi wa mto Jordan kwenye operesheni iliyofanywa jana usiku.

    Kamati hiyo imetoa taarifa ikisema, operesheni hiyo inalenga kuhakikisha kuwa mapigano yanayohusisha Hekalu Tukufu la Mount hayatapamba moto.

    Ingawa kundi la Hamas halikuhusika na ufyatuaji risasi uliotokea Julai 14 katika hekalu hilo lililoko katika mji mkongwe wa Jerusalem, lakini kundi hilo limesifia shambulizi hilo kuwa ni la kishujaa na muhimu, huku likiwachochea waislamu kuendelea na maandamano yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako