• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka India kuondoa haraka wanajeshi wake waliovamia eneo la China

    (GMT+08:00) 2017-07-24 19:31:16

    China imeitaka India kuondoa haraka wanajeshi wote walioingia China kinyume cha sheria, na kusema taifa litalinda maeneo yake kwa gharama yoyote ile.

    Akiongea na wanahabari kuhusiana na wanajeshi wa India waliovuka mpaka na kuingia eneo la China katikati ya mwezi Juni ili kuzuia ujenzi wa barabara katika mkoa wa Donglang, msemaji wa Wizara ya Ulinzi wa taifa Wu Qian, amesema askari wa mpakani wa China wamechukua hatua za awali za kukabiliana na hali katika eneo hilo na wataongeza usambazaji wa askari na mazoezi. Akitoa wito wa kufanyika kwa juhudi za pamoja ili kudumisha amani maeneo ya mpakani, Bw. Wu ameitaka India kuchukua hatua imara za kusahihisha makosa yake na kuacha uchokozi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako