Ripoti imesema Kutobadilika kwa makadirio hayo kunatokana na sababu tofauti kwa mujibu wa nchi, ambapo kimsingi inaonesha ni matokeo ya kubadili sera za uchumi katika nchi mbili zenye uchumi mkubwa, Marekani na China.
Ripoti imekadiria kuwa ukuaji wa uchumi wa China kwa mwaka 2017 utapanda kwa asilimia 0.1 na kufikia asilimia 6.7 kutoka Aprili, ikionesha uimara katika robo ya kwanza. Kwa upande wa Marekani makadirio yanaonesha kushuka kutoka asilimia 2.3 ahadi 2.1 mwaka huu, na kutoka asilimia 2.5 hadi 2.1 mwaka 2018. Ripoti imesema nchi nyingine yenye ukuaji mdogo ni Uingereza ukiwa na ukuaji dhaifu kuliko ilivyotarajiwa katika robo ya kwanza.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |