• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Unga wa mahindi umerudi madukani

    (GMT+08:00) 2017-07-24 20:07:47

    Kuboreka kwa usambazaji wa unga wa mahindi katika maduka kumeleta afueni kwa wapenzi wa bidhaa hiyo, huku wauzaji wakisema wasagaji wanasambaza bidhaa hiyo kwa wakati kinyume na wiki chache zilizopita.

    Wauzaji wengine sasa wanaruhusu wateja kununua zaidi ya pakiti mbili kinyume na hapo awali, ambapo mtu walikubaliwa kununua pakiti mbili pekee.

    Waziri wa Kilimo Willy Bett alikuwa amesema mapema wiki iliyopita hali itabadilika ndani ya wiki mbili.

    Bett alitoa matangazo hayo akipokea mifuko 335, 000 ya mahindi kutoka Mexico kwenye bandari ya Mombasa wiki iliyopita.

    Aidha amesema Meli tatu zaidi zilitarajiwa kufika Ijumaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako