• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Polisi nchini Kenya wakamata vinara saba wa dawa za kulevya Mombasa

    (GMT+08:00) 2017-07-25 09:09:43

    Makachero wa kupambana na dawa za kulevya nchini Kenya wamekamata vinara saba wa dawa za kulevya wanaosakwa katika kaunti ya Mombasa. Kamanda wa polisi wa kanda hiyo Bw. Larry Kieng amesema makachero hao pia walikamata magari saba yaliyofichwa katika nyumba moja kwenye vitongoji vya Nyali, na pesa taslim za Kenya na Marekani zinazoaminika kuwa ni mapato ya biashara ya dawa za kulevya. Bw. Kieng amesema hivi sasa polisi wanawahoji washukiwa hao baada ya mahakama kuwapa polisi siku tano kumaliza uchunguzi wao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako