• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Virusi vya Ukimwi kwa mtoto mmoja Afrika Kusini vyaonekana kupungua bila matumizi ya dawa

    (GMT+08:00) 2017-07-25 09:38:01

    Idara ya taifa ya afya ya Marekani NIH imesema mtoto mwa miaka 9 aliyegunduliwa kuwa na virusi vya ukimwi akiwa na mwezi mmoja, na kupatiwa dawa ya kupambana na virusi hivyo akiwa mchanga, ameweza kutuliza virusi hivyo kwa muda wa miaka nane na nusu bila kutumia dawa.

    Mkurugenzi wa NIH Bw Anthony Fauci amesema hali hii inaimarisha imani kuwa kama watoto wachanga wakipatiwa matibabu, wanaweza kuepushwa kupata tiba ya muda mrefu na kuamshwa kwa kinga mwili ya kupambana na virusi.

    Kumekuwepo na tafiti kadhaa kuhusu watoto wenye virusi vya Ukimwi kupatiwa matibabu siku chache baada ya kuzaliwa, na kuwa na matokeo ya kuridhisha. Baadhi ya watoto walionyesha kudhibiti kwa kiwango kikubwa kuongezeka kwa virusi wa ukimwi mwilini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako