• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kundi la Al-Shabaab lashambulia msafara wa vikosi vya AU kusini mwa Somalia

    (GMT+08:00) 2017-07-25 09:45:03

    Kundi la Al-Shabaab jana lilivamia msafara wa vikosi vya jeshi la Umoja wa Afrika na Somalia katika mkoa wa Gedo kusini mwa Somalia, hata hivyo hakuna vifo vilivyoripotiwa na jeshi hilo.

    Kamanda wa jeshi la Somalia mkoani Gedo Shukri Abdullahi amesema, wanamgambo hao walitega mabomu kando ya barabara inayotumiwa na vikosi hivyo katika mji wa Bardhere, na baada ya jeshi kupambana na wanamgambo hao askari mmoja alijeruhiwa kidogo.

    Kwa mujibu wa mwenyeji wa huko, mapambano yalikuwa yakisikika hadi nje ya mji wa Bardhere, hata hivyo hivi sasa hali imekuwa ya kawaida.

    Kundi la Al-shabaab limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako