• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Afrika wafikiria kukabidhi majukumu ya usalama kwa vikosi vya Somalia

    (GMT+08:00) 2017-07-25 09:55:34

    Tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM na serikali ya Somalia jana mjini Mogadishu zilianza mkutano wa siku nne, kujadili njia za kukabidhi majukumu ya usalama kutoka kwa vikosi vya AMISOM kwenda kwa jeshi la Somalia .

    Akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo, mwakilishi maalum wa mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (SRCC) ya Somalia, Bw Francisco Maderia amesisitiza umuhimu wa kuwezesha vikosi vya usalama wa kitaifa wa Somalia (SNSF), kuviimarisha kwa ufanisi na kuhakikisha mchakato wa mpito unaenda vizuri.

    Madeira amesema swali lililopo ni jinsi Serikali ya Somalia, AMISOM na vikosi vya usalama wa kitaifa vya Somalia vitakavyohusika na maamuzi haya, na mapendekezo na kile wanachohitaji kufanya kutekeleza maamuzi haya ili kuyafanikisha.

    Mkutano huo utajadili kwa undani utekelezaji wa usanifu wa usalama wa taifa unaotokana na mkataba wa usalama uliosainiwa na viongozi wa Somalia Aprili 16.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako