• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IMF yasema China itaendelea kuwa injini kuu ya uchumi wa dunia

    (GMT+08:00) 2017-07-25 10:04:15

    Shirika la Fedha la Kimataifa IMF limetoa ripoti mpya kuhusu uchumi wa dunia mjini Kuala Lumpur, Malaysia na kupandisha tena makadirio yake kuhusu ongezeko la uchumi wa China kwa mwaka huu na mwakani.

    Mchumi mkuu wa IMF Bw Maurice Obstfeld amesema, China inachangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa uchumi wa dunia, na itaendelea kuwa injini kuu ya uchumi wa dunia.

    Bw Obstfeld anaona kuwa uchumi wa China umeongezeka kwa nguvu katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, na ongezeko la asilimia 6.9 katika robo ya pili ya mwaka huu limezidi makadirio. Pia ameipongeza China kwa juhudi zake kwenye kuhimiza utandawazi wa dunia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako