• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yatumai pande mbalimbali zichukue fursa kuhimiza mazungumzo kuhusu suala la Syria

    (GMT+08:00) 2017-07-25 10:14:33

    Mjumbe maalumu wa China anayeshughulikia suala la Syria Bw. Xie Xiaoyan, amesema hivi sasa mabadiliko muhimu yametokea katika hali ya Syria, na pande mbalimbali zinapaswa kutumia fursa hii kuhimiza mazungumzo, ili kuweka msingi wa kutatua mgogoro wa Syria kwa njia ya kisiasa.

    Bw. Xie Xiaoyan ambaye yuko ziarani nchini Uturuki, amewaambia waandishi wa habari kuwa, hivi karibuni baadhi ya nchi zilizoko nje ya kanda hiyo zimebadilisha msimamo kuhusu suala la Syria, kauli na vitendo vyao vitasaidia utatuzi wa suala hilo, na kuhimiza pande mbalimbali kufanya mazungumzo.

    Habari kutoka Syria zinasema muungano wa kimataifa wa kupambana na kundi la IS unaoongozwa na Marekani umefanya shambulizi la anga dhidi ya gereza linalodhibitiwa na IS, na kusababisha vifo vya raia wasiopungua 30 ndani ya gereza hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako