• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Hatima ya Kocha Micho bado haijulikani

    (GMT+08:00) 2017-07-25 10:24:30
    Shirikisho la soka nchini Uganda FUFA imeshindwa kubainisha iwapo mkufunzi wa timu ya soka ya Uganda Cranes Micho Sredojevic ataendelea na majukumu yake kama kocha au la.

    FUFA ilitarajiwa kutoa mwelekeo kuhusu hatma ya kocha huyo hapo jana lakini ikatoa taarifa tu kusema mazungumzo baina yake na Micho bado yanaendelea, huku wakala wa kocha huyo akidokeza kuwa uamuzi huo utafanywa karibuni.

    Wikendi iliyopita, Micho alitangaza nia yake ya kutoendelea kuifunza timu ya Cranes kutokana na kutokuelewana baina yake na usimamizi wa soka nchini humo akidai kuwa malimbikizo yake hayajashughulikiwa ipasavyo na shirikisho la soka nchini Uganda FUFA.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako