• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchumi wa viwanda wa China wadumisha mwelekeo mzuri

    (GMT+08:00) 2017-07-25 18:15:00

    Mkurugenzi wa Idara ya uratibu ya uendeshaji na usimamizi kwenye Wizara ya viwanda na upashanaji wa habari ya China Bw. Zheng Lixin amesema, uchumi wa viwanda umedumisha mwelekeo mzuri nchini China.

    Hayo amesema katika mkutano wa Ofisi ya habari katika baraza la serikali la China. Ameeleza kuwa, katika nusu ya kwanza ya mwaka huu, thamani ya ongezeko la viwanda ambavyo vina mapato ya biashara imezidi yuan milioni 20 kwa mwaka na kuongezeka kwa asilimia 6.9 ikilinganishwa na mwaka jana wakati kama huu, hali ambayo ni nzuri zaidi katika miaka mitatu iliyopita. Inakadiriwa kuwa mwelekeo huo utadumu katika nusu ya pili mwaka huu.

    Bw. Zheng pia amesisitiza kuwa inatakiwa kuimarisha usimamizi na upimaji kuhusu uendeshaji wa viwanda na makadirio kuhusu utoaji wa tahadhari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako