• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Umoja wa Mataifa walaani tukio la kushambuliwa kwa tume yake ya kulinda amani nchini Afrika ya Kati

    (GMT+08:00) 2017-07-25 18:34:22

    Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antoni Guterres jana kwa nyakati tofauti walitoa taarifa wakilaani waasi wa kundi la kikristo laanti-Balaka kushambulia askari wa ulinzi wa amani wa tume ya kulinda amani nchini Afrika ya Kati huko Bangassou. Shambulizi hilo lilisababisha kifo cha askari mmoja raia wa Morocco na wengine watatu kujeruhiwa.

    Kwenye taarifa hiyo Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lilisema kuwashambulia askari wa ulinzi wa amani kunaweza kuhukumiwa kuwa ni uhalifu wa kivita, na kuzitaka pande zote zitekeleze sheria ya ubinadamu ya kimataifa, likiisisitiza serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati ianze kufanya uchunguzi na kuwaadhibu washambuliaji.

    Naye katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa alitoa taarifa kupitia msemaji wake akizitaka pande zote zisimamishe vitendo vya mabavu, na kuunga mkono juhudi za tume yake ya kulinda amani kwa kuwalinda raia na kuisaidia Afrika ya Kati kulinda usalama wake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako