• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Taliban yadhibiti wilaya ya Jani Khil nchini Afghanistan

    (GMT+08:00) 2017-07-25 18:52:25

    Televisheni ya Tolo nchini Afghanistan imeripoti kuwa, baada ya mapambano makali ya siku kadhaa wanamgambo wa Taliban leo asubuhi wamedhibiti eneo la katikati ya wilaya ya Jani Khil mkoa wa mashariki wa Paktia.

    Kwa mujibu wa Zabihullah Majahid anayedai kuwa msemaji wa Taliban, wapiganaji hao sasa tayari wameshaweka kambi katika makao makuu ya polisi wilayani Jan Khil.

    Wakati huohuo, waziri wa mambo ya ndani ametoa taarifa akikanusha habari hizo na kusisitiza kuwa Vikosi vya Ulinzi na Usalama vipo kwenye eneo la mapambano na mapigano bado yanaendelea. Katika wiki zilizopita wanamgambo wa Taliban wamedhibiti wilaya ya Kohistanat na Taiward mkoani Ghor.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako