• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ongezeko la hatua za uwekaji vizuizi vya kibiashara lashuka zaidi tokea mwaka 2008

    (GMT+08:00) 2017-07-25 18:54:49

    Ripoti iliyotangazwa jana na Shirika la biashara duniani WTO imeonesha kuwa, kuanzia katikati ya mwezi Oktoba mwaka jana hadi katikati ya mwezi Mei mwaka huu, nchi wanachama wa shirika hilo wametekeleza hatua 74 za uwekaji wa vizuizi vya kibiashara, idadi ambayo imeshuka zaidi tangu msukosuko wa fedha ulipotokea mwaka 2008.

    Hatua hizo ni pamoja na kutoza au kuongeza ushuru wa forodha na kuongeza nguvu katika usimamizi wa forodha.

    Katibu mkuu wa WTO Bw. Roberto Azevedo anaona kuwa, ripoti hiyo imeonesha juhudi za nchi wanachama wa WTO katika kuboresha mazingira ya biashara duniani. Pia amezihimiza nchi wanachama wa shirika hilo kujizuia kutekeleza hatua za kuweka vizuizi vya kibiashara wakati zikikabiliana na hali isiyo imara ya uchumi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako