• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-URA yakosa kufikia malengo

    (GMT+08:00) 2017-07-25 19:18:17

    Mamlaka ya mapato Uganda (URA) imekosa kufikia malengo yake ya Sh13 trilioni kwa mwaka wa fedha 2016/2017 kwa sh457.51bn.

    Haya yalisemwa jana na Kamishna Mkuu wa mamlaka ya mapato URA Margaret Okal.

    Bi Okal alisema malengo hayo yamekosa kufikiwa kutokana na utendaji mdogo wa kiuchumi.

    Shirika la Fedha Duniani mwezi Mei lilitabiri ukuaji wa uchumi wa asilimia 3.5 kutoka asilimia 5 ambayo lilitabiri hapo awali,likisema kuwa nchi hiyo haitapata ukuaji mkubwa wa kiuchumi kutokana na kupanda kwa bei ya chakula kutokana na ukame wa muda mrefu.

    Aidha Bi Okal alisema mikopo midogo iliyotolewa kwa sekta binafsi katika mwaka wa fedha uliopita iliathiri sana viwanda,maduka ya jumla na rejareja,na ujenzi,na hatimaye kupunguza ukusanyaji wa mapato ya ndani kutokana na ushuru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako