• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Serikali ya Afrika Kusini yakanusha kuondoa amri ya kupiga marufuku ya biashara ya pembe za faru

    (GMT+08:00) 2017-07-25 19:26:11

    Waziri wa mazingira wa Afrika Kusini Bibi Edna Molewa amekanusha ripoti ya vyombo vya habari kuhusu Afrika Kusini kuondoa amri ya kupiga marufuku biashara ya pembe za faru, huku akisema, serikali ya nchi hiyo itafuata kwa makini makubaliano ya biashara za kimataifa za wanyama na mimea pori iliyoko hatarini na kuendelea kupiga marufuku biashara za kimataifa za pembe za faru.

    Kutokana na vifo vya faru wengi, serikali ya Afrika Kusini mwaka 2009 ilisimamisha biashara za pembe za faru. Wafugaji wa faru wa nchi hiyo wanataka kuondolewa kwa amri hiyo, ambapo wanaona haiwezi kuzuia kuwawinda faru na kukata rufaa mahakamani.

    Mwaka jana, mahakama moja ilitoa hukumu kuwa amri ya serikali haina uhalali. Mwezi Aprili mwaka huu, mahakama kuu ilikataa rufaa ya serikali kutaka kuendelea kupiga marufuku biashara za pembe za faru. Hata hivyo Bibi Molewa amesema, hukumu ya mahakama kuu inafaa kwa biashara za ndani, lakini wafanyabiashara wa ndani wa pembe za faru pia wanatakiwa kupata kibali kinachotolewa na serikali na kufikia vigezo vingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako