• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uingereza kufanya mazungumzo kuhusu makubaliano ya biashara huria na Ulaya na Marekani

    (GMT+08:00) 2017-07-25 19:27:18

    Waziri wa biashara za kimataifa wa Uingereza Bw. Liam Fox amesema, baada ya kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, nchi hiyo itafanya mazungumzo kuhusu makubalino ya biashara huria na Umoja wa Mataifa na Marekani.

    Akitoa hotuba katika taasisi ya kampuni za Marekani huko Washington Bw. Fox amesema , baada ya kujitoa Umoja wa Ulaya Uingereza itatafuta kujenga uhusiano wa kibiashara wa pande zote na nchi za umoja huo.

    Pia amedokeza kuwa Uingereza na Marekani zimejenga kikundi cha biashara na uwekezaji. Kikundi hicho kitajadili jinsi Uingereza itakavyohakikisha shughuli za kibiashara zinadumu baada kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya, ili kutoa utulivu, uhakikishaji na imani kwa kampuni za nchi hizo mbili, huku kikijenga msingi wa kufikia makubaliano ya biashara huria kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako