• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ukuaji wa GDP wa China wakadiriwa kufikia asilimia 6.8 kwa mwaka huu

    (GMT+08:00) 2017-07-25 19:42:38

    Taasisi mbili za China leo zimetoa makadirio ya ukuaji wa pato la taifa GDP la China na kusema litafikia asilimia 6.8 mwaka huu, likipungua kidogo kuliko nusu ya kwanza iliyokuwa na asilimia 6.9, hata hivyo kwa mujibu wa lengo la mwaka la asilimia 6.5 litakuwa limepanda.

    Taasisi ya Elimu ya Sayansi ya Jamii ya China imesema kwenye ripoti yake kuwa ukuaji katika robo ya 3 na 4 utakuwa asilimia 6.8 na 6.7, ambapo uwekezaji, matumizi na usafirishaji nje vinaweza kukua kwa kiwango kidogo. Taasisi hiyo imesisitiza kuwa uchumi wa China utaendelea kukua kwa utulivu na kwamba ina uhakika kuhusu kufikia malengo ya ukuaji wa mwaka.

    Nacho Kituo cha Habari cha Taifa kimetoa makadirio sawa kuhusu ukuaji wa uchumi wa mwaka, na kusema katika nusu ya mwisho utakua kwa asilimia 6.7

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako