• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wapalestina waandamana kupinga hatua za kiusalama zilizowekwa na Israel katika msikiti wa Al-Aqsa

  (GMT+08:00) 2017-07-26 10:01:59

  Hali ya wasiwasi inaendelea katika Ukingo wa Magharibi na Jerusalem ya mashariki, baada ya Israel kuweka vifaa vipya vya usalama katika lango la msikiti wa Al-Aqsa tangu tarehe 14 Julai.

  Wapalestina wanaendelea kuandamana katika sehemu mbalimbali za Jerusalem mashariki na Ukingo wa Magharibi, na kupambana na vikosi vya Israel kupinga hatua hiyo.

  Rais Mahmoud Abbas wa Palestina amesisitiza kuwa, hali ya msikiti huo inapaswa kurejeshwa kuwa kama ilivyokuwa kabla ya tarehe 14 Julai.

  Na hivi karibuni Jordan pia imeingilia mgogoro kati ya Israel na Palestina. Habari nyingine zinasema waziri wa mambo ya nje wa Jordan Bw Ayman Safadi amesema, Jordan na Israel hazikufanya mazungumzo kuhusu tukio la ufyatuaji risasi nje ya ubalozi wa Israel nchini Jordan lililosababisha vifo vya wajordan wawili. Amesema tukio hilo ni kesi ya jinai inayoshguhulikiwa kwa mujibu wa sheria. Ameongeza kuwa, Jordan inasisitiza kumhoji mwisraeli aliyewauawa wajordan wawili, lakini Israel inakataa kwa sababu ya kinga ya kidiplomasia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako