• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Viongozi wa Libya wakubali kusimamisha uadui kwa ajili ya uchaguzi wa urais

    (GMT+08:00) 2017-07-26 10:13:13

    Waziri Mkuu wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Libya Bw Fayez Al Sarraj na kamanda wa Jeshi la Taifa la Libya Bw Khalifa Haftar jana wamekutana mjini Paris, na kutoa taarifa ya pamoja kwamba pande mbili zitasimamisha vita na kuweka mazingira ya amani kwa ajili ya uchaguzi wa urais na wa bunge.

    Taarifa hiyo imesema kwamba pande zote mbili zimefikia makubaliano kuhusu kutatua mgogoro wa Libya kwa njia ya kisiasa ili kupata maafikiano ya kitaifa. Pia zimeahidi kusitisha vita na kutotumia nguvu, kwa mujibu wa makubaliano ya kisiasa ya Libya na ya kimataifa yaliyofikiwa.

    Taarifa pia imesema kuwa pande zote mbili zitaunga mkono katika kuijenga Libya kuwa nchi yenye amani, demokrasia na utawala wa kisheria, na kuwezesha makabidhiano ya madaraka kwa njia ya amani na kujenga taasisi za serikali ya umoja, pia kutekeleza kithabiti Makubaliano ya kisaisa ya Libya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako