• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tume ya uchaguzi ya Kenya yakamilisha maandalizi ya uchaguzi wa Agosti

    (GMT+08:00) 2017-07-26 10:19:20

    Tume huru ya uchaguzi na mipaka ya Kenya IEBC imesema iko katika hatua za mwisho kukamilisha miundombinu na mafunzo ya wafanyakazi kwa ajili ya uchaguzi mkuu utakaofanyika Agosti 8.

    Mwenyekiti wa tume hiyo Bw Ezra Chiloba amewaambia waandishi wa habari mjini Nairobi kuwa uchapishaji wa karatasi za kupigia kura umemalizika.

    Bw Chiloba pia amewahakikishia wakenya na wadau mbalimbali kuwa, miundombinu na timu ya wafanyakazi kwa ajili ya uchaguzi viko tayari, na majaribio ya vifaa vya kidigitali ambavyo vitatumika kupitisha matokeo ya uchaguzi yanaendelea, na vitasambazwa kwenye vituo vya kupigia kura zaidi ya 40,000 nchini kote.

    Wakenya wanatarajia kupiga kura kuchagua rais, wabunge, wakuu wa Kaunti na madiwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako