• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yazitaka pande husika kujizuia katika suala la Peninsula ya Korea

    (GMT+08:00) 2017-07-26 19:18:51

    Msemaji wa Wizara ya mambo nje ya China Bw. Lu Kang amesema, hivi sasa hali ya Peninsula ya Korea inakabiliwa na changamoto kubwa, China inapinga kithabiti kitendo chochote kinachoongeza hali ya wasiwasi na kuzitaka pande husika kuzingatia hali ya amani na utulivu wa peninsula hiyo, kujizuia na kufanya juhudi ya kiujenzi katika kulegeza hali ya wasiwasi ya peninsula hiyo.

    Bw. Lu alisema hayo wakati akizungumzia taarifa kutoka vyombo vya habari vya Marekani kuhusu Korea Kusini kurusha tena kombora la jaribio. Bw. Lu amesisitiza kuwa China siku zote inapendekeza kutimiza hali ya kutokuwa na silaha za kinyuklia katika peninsula ya Korea, huku ikilinda kithabiti amani na utulivu wa peninsula hiyo.

    Pia amesema, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa azimio kuhusu shughuli ya kurusha makombora ya Korea Kusini, na China inapinga kithabiti kitendo chochote kinachokiuka azimio la baraza hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako