• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Kenya inahitaji trilioni moja kila mwaka ujenga miundo mbinu bora ya maji, uchukuzi na mawasiliano.

    (GMT+08:00) 2017-07-26 19:27:29

    Kenya inahitaji shilingi trilioni moja kila mwaka ili kujenga miundo mbinu bora ya maji, uchukuzi na mawasiliano.

    Ripoti ya G20 kuhusu tathmini ya uwekezaji wa miundo mbinu duniani inaonyesha kwamba Kenya itahitaji hadi dola bilioni 206 ndani ya miaka 23 ijayo ili kutimiza mahitaji ya miundo mbinu yake.

    Ripoti hiyo inatoa wito kwa Kenya kuongeza uwekezaji kwenye miundo mbinu kwa asilimia 41 ili kukidhi mahitaji yake mwaka 2040 na pia kufikia malengo ya maendeleo endelevu ya milenia.

    Idadi ya watu nchini Kenya inatarajiwa kuongezeka kwa watu milioni 35 ifikapo mwaka wa 2040 huku nao uchumi ukikua kwa asilimia 5.5.

    Aidha ripti hiyo inasema Kenya inaghitaji pesa zingingine dola bilioni 31o ili kuwezesha Kenya kufikia lengo la milenia la kuwa na maji safi na kawi ya kutosha.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako