• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: URA yaweka malengo mapya ya kukusanya ushuru Uganda

    (GMT+08:00) 2017-07-26 19:28:33

    Mamlaka ya kukusanya ushuru nchini Uganda imesema sababu za kukosa kutimiza lengo lake la ukusanyaji wa mapato ni Uganda kupungua kwa utenda kazi kwenye sekta ya utengenezaji bidhaa.

    Mamlaka hiyo imekuwa na upungufu wa shilingi bilioni 458 kwenye kipindi cha mwaka wa fedha 2016/12.

    Pesa hizo zinazopungua zinatosha kufadhili bajeti ya bunge kwa kipindi cha mwaka mzima.

    Kamishena wa URA Doris Akol amesema ukuaji wa uchumi umekua kwa asilimia 3.9 licha ya matarajio ya ukuaji wa asilimia 5.

    Uachumi wa Uganda ulikuwa na ukuaji wa pole pole hasa kutokana na kiangazi ambacho kilipelekea kupanda kwa bei ya vyakula.

    Hata hivyo sasa Akol anasema URA inalenga kukusanya shilingi trillion 15 kwenye kipindi cha fedha cha 2017/18.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako