• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Magufuli amezindua barabara ya kilometa 707

    (GMT+08:00) 2017-07-26 19:30:53

    Rais wa Tanzania John Magufuli amezindua barabara ya kilometa 707 zinazounganisha mikoa ya mikoa ya Ukanda wa Kati na Magharibi zilizojengwa kwa lami kwa gharama ya Sh bilioni 860.

    Sherehe za uzinduzi wa miradi hiyo ya barabara zilifanyika katika mikoa ya Kagera, Kigoma, Tabora na kuhitimishwa jana mkoani Singida. Uzinduzi wa barabara hizo unafungua fursa sasa kwa mikoa hiyo katika nyanja mbalimbali za kiuchumi na kijamii si kwa Tanzania pekee, bali pia kuiunganisha mikoa hiyo na nchi za jirani.

    Akizungumza na wananchi wa Itigi mkoani Singida katika sherehe za uzinduzi wa barabara ya Manyoni-Itigi-Chaya yenye urefu wa kilometa 89.3 Rais John Magufuli alisema serikali yake imedhamiria kuhakikisha mtandao wa barabara kuu nchi nzima unaboreshwa na zote kuwa na kiwango cha lami.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako