• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lafanya mkutano kuhusu suala la Palestina

    (GMT+08:00) 2017-07-26 19:32:09

    Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa lilikutana jana na kujadili suala la Palestina, mwenyekiti wa zamu wa mwezi huu wa baraza la usalama ambaye pia ni mjumbe wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Liu Jieyi aliongoza mkutano huo.

    Msimamizi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati Bw. Nickolay Mladenov alisema hali ya Palestina na Israel imezidi kuwa mbaya na huenda mgogoro kati yao ukawa mgogoro wa kidini. Alizitaka pande zote kuacha vitendo vya uchochezi na kujizuia ili kutatua mgogoro huo haraka iwezekanavyo.

    Bw. Liu Jieyi pia alieleza mapendekezo manne yaliyotolewa na rais Xi Jinping wa China kuhusu utatuzi wa suala la Palestina, yakiwemo kuhimiza kutatua suala hilo kwenye msingi wa mpango wa nchi mbili, kushikilia maoni ya pamoja, kina, ushirikiano na endelevu kuhusu usalama, kuratibu juhudi ya jumuiya ya kimataifa, kuongeza nguvu ya kuhimiza amani, na kutekeleza sera kwa kina.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako