• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yapitisha pendekezo la kuweka vikwazo dhidi ya Russia, Iran na Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2017-07-26 19:35:39

    Baraza la chini la Bunge la Marekani limepitisha pendekezo la kuweka vikwazo dhidi ya nchi tatu zikiwemo Russia, Iran na Korea Kaskazini.

    Pendekezo hilo limepitishwa kwa kura 419 za ndiyo na nyingine tatu za hapana. Kwa mujibu wa pendekezo hilo, Marekani itaongeza vikwazo vya kiuchumi kwa watu na mashirika husika ya Russia kwa kisingizio cha tuhuma ya Russia kuingilia katika uchaguzi mkuu wa Marekani wa mwaka 2016 na mgogoro wa Ukraine, huku ikiweka vikwazo dhidi ya Iran na Korea Kaskazini kutokana na miradi ya kuendeleza makombora ya msafa marefu.

    Habari nyingine kutoka shirika la habari la taifa la Iran IRNA limesema, mjumbe mwandamizi wa mazungumzo ya nyuklia wa Iran ambaye pia ni naibu waziri wa mambo ya nje wa nchi hiyo Bw. Abbas Araqchi amesema, vikwazo vipya vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Iran vitaleta athari mbaya katika utekelezaji wenye mafanikio wa makubaliano ya kinyuklia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako