• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mapato ya sekta ya utalii Tanzania yanatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 30

    (GMT+08:00) 2017-07-27 09:33:54

    Mapato kutokana na sekta ya utalii nchini Tanzania yanatarajiwa kuongezeka kwa asilimia 30, kufuatia ongezeko kubwa la idadi ya watalii waliotembelea Tanzania kwa mwaka huu.

    Waziri wa maliasili na utalii wa Tanzania Profesa Jumanne Maghembe amesema ameshuhudia mwenyewe kushamiri kwa sekta ya utalii, na kusema hadi kufikia Agosti 29 mwaka huu karibu nafasi zote kwa ajili ya watalii zimejaa.

    Pia amesema Tanzania imekuwa na bahati kubwa kwani watu maarufu wamefanya utalii nchini Tanzania, na kusaidia kuitangaza Tanzania nje ya nchi.

    Hata hivyo Bw Maghembe amesema baadhi ya barabara za kuelekea kwenye vivutio vya utalii ziko katika hali mbaya, ameahidi kuwa serikali itajitahidi kukarabati barabara hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako