• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mazungumzo ya 13 ya usalama wa kimkakati kati ya China na Russia yafanyika Beijing

  (GMT+08:00) 2017-07-27 10:27:55

  Mjumbe wa taifa wa China Bw. Yang Jiechi na katibu wa kamati ya usalama ya Russia Nikolai Patrushev jana hapa Beijing wameendesha kwa pamoja mazungumzo ya 13 ya usalama wa kimkakati kati ya China na Russia.

  Bw. Yang Jiechi amesema, pande hizo mbili zinapaswa kutekeleza kwa makini makubaliano yaliyofikiwa na marais wa nchi hizo, kuimarisha zaidi uaminifu na uratibu wa kimkakati, na ushirikiano wa usalama. Pia amesema pande mbili zinatakiwa kulinda maslahi ya pamoja ya usalama wa kimkakati, ili kuweka mazingira salama na tulivu kwa ajili ya kujiendeleza, na kuhimiza amani, utulivu na maendeleo ya kikanda na ya dunia nzima.

  Kwa upande wake Bw. Patrushev amesema kuendeleza uhusiano wa kiwenzi na kimkakati kati ya China na Russia ni jambo linalopewa kipaumbele katika diplomasia ya Russia. Amesema Russia na China zinapaswa kuendelea kuungana mkono, na kulinda kwa pamoja utulivu wa kisiasa na kimkakati wa nchi hizo mbili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako