Wabunge walisema Emong aliiletea Uganda sifa baada ya kumpiku bingwa mtetezi Samir Nouioua kutoka Algeria.
Mbunge wa kaunti ya Kioga Anthony Okello, aliwasilisha hoja bungeni kushinikiza kutambuliwa kwa Emong wakati wa kikao cha jana. Hoja hiyo iliungwa mkono na wabunge wengi ambao walitoa wito kwa serikali kujenga nyumba kwa Emong na pia kununua gari kwa ajili yake jinsi ilivyofanyika kwa wanariadha wengine kama vile bingwa wa riadha duniani mwaka 2013 Stephen Kiprotich.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |