• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Monacco yakatisha tamaa uamisho wa Mbappe

    (GMT+08:00) 2017-07-27 10:32:11
    Klabu ya Monaco imeanza mazungumzo ya kumuongezea kandarasi mshambuliaji wake Kylian Mbappe kulingana na makamu wa rais wa klabu hiyo Vadim Vaslyev.

    Mbappe ambaye ana kandarasi hadi mwezi juni 2019 amehusishwa na uhamisho wa Real Madrid. Manchester City, Paris Saint Germain na Arsenal pia zimehusishwa, lakini duru zinasema kwamba vilabu hivyo haviko tayari kulipa kitita cha Yuro milioni 180 za uhamisho wa mchezaji huo.

    Mchezaji huyo kutoka Ufaranza aliifungia Monaco mabao 26 katika mashindano yote msimu uliopita.

    Mapema mwezi Julai Monaco ilisema vilabu muhimu kutoka Ulaya viliwasiliana na mchezaji huyo bila ruhusa yao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako