• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Uzalishaji wa mafuta kuendelea hadi mwisho wa 2017

    (GMT+08:00) 2017-07-27 18:52:26
    Kampuni ya uchimbaji mafuta ya Tullow imearifu kuwa uzalishaji wa mafuta ulioharishwa mwezi uliopita utaendelea mwishoni mwa mwaka huu.

    Serikali ya Kenya ililazimika kuahirisha uzalishaji huo uliopangwa kuanza juni mwaka huu.

    Katika ripoti yao kwa vyombo vya habari,uzalishaji wa mafuta mapipa 2000 ya mafuta kwa siku kwa majaribio utaanza mwisho wa mwaka.

    Mafuta ya kwanza yaliochimbwa mwaka 2015 yatasafirishwa baada ya majaribio na kupitia Turkana hadi Mombasa .

    Waziri wa kawi Charles Keter amesema serikali imeamua kuahirisha uzalishaji hadi pale bunge litakapojadili na kupitisha sheria kuhusiana na ugavi wa mapato ya mafuta.

    Kumekua na changamoto kama suala la usalama duni katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa nchi haswa kuhusu miundo msingi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako