• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Serikali kuendeleza unga wa bei nafuu

    (GMT+08:00) 2017-07-27 18:52:46

    Wakenya wataendelea kununua unga wa sima bei rahisi ya shilingi 90 kwa kilo mbili baada ya serikali kutangaza kuongeza mda wa ruzuku ya unga .

    Waziri wa kilimo nchini Kenya Willy Bett amesema ruzuku hiyo itaendelea hadi mwezi Septemba mwaka huu pale wakulima watakapokamilisha mavuno ya mahindi.

    Waziri Bett amesema licha ya Kenya kupata mahindi mwaka huu,takwimu zinaonyesha kwamba ikilinganishwa na mavuno ya mwaka uliopita Kenya ina kasoro ya asilimia 15 ya mahindi.

    Mapema mwaka huu Kenya iliagiza mahindi kutoka nje na kuyanunua kwa shilingi 2300 kwa gunia bei iliopelekea wauzaji kuuza nafuu kwa wateja wao kwa jumla.

    Serikali aidha imesema hata baada ya biashara ya mahindi kuregea katika hali ya kawaida kilo mbili ya unga wa sima haitauzwa kwa zaidi ya shilingi 100.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako