• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:China kujenga kiwanda cha saruji cha trilioni 1,8 Kampala

    (GMT+08:00) 2017-07-27 18:53:48
    China imepewa zabuni ya kujenga kiwanda cha saruji cha thamani ya shilingi trilioni 1.8 katika jiji la Kampala Uganda.

    Kiwanda hicho kitajegwa na kampuni ya SINOMA ya China inayojenga viwanda vingine katika mji wa Tanga Tanzania.

    Liu Zhijiang mwenyekiti wa kiwanda hicho amesema mradi huu utajengwa baada ya kukamilika kwa makubaliano baina yao na serikali ya Uganda.

    Kiwanda hiki ni kutokana na ziara ya wajumbe wa Uganda nchini China waliokubaliana kufanya mikakati ya kuimarisha ushirikiano wa kibiashara baina ya nchi hizi mbili.

    Utafiti wa mwaka 2011 uliofanywa na kitengo cha madini na masuala ya jiologia ,eneo la karamoja jijini Kampala liligundua madini kama Uranium,Wolfram,Graphite ,shaba na Lithium.

    Mradi huu unatarajiwa kubuni ajira ya zaidi ya watu 3000 na kupunguza bei ya gunia la simiti ambalo kwa sasa kilo 50 ya saruji inauzwa elfu 36.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako