• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuanza majaribio ya kurejesha kasi ya treni ya mwendo kasi kwa kilomita 350 kwa saa

    (GMT+08:00) 2017-07-27 19:42:29

    China leo imeanza majaribio ya kurejesha kasi ya juu ya treni ya kasi ya reli ya kati ya Beijing na Shanghai hadi kufikia kilomita 350 kwa saa, ikiwa ni miaka sita baada ya kupunguza hadi kilomita 300 kwa saa.

    Ikiondoka katika kituo cha treni cha Beijing saa 2:38 asubuhi treni ya kasi ya Fuxing itakamilisha safari yake ya kwenda na kurudi kutoka Beijing hadi Xuzhou iliyoko umbali wa kilomita 700 ndani ya saa 4. Kuongezwa kwa kasi hiyo kutapunguza muda wa safari kwa saa 4.50, ambapo itakuwa na kasi kwa nusu saa zaidi kuliko ya sasa kati ya miji hiyo miwili. Kama majaribio hayo yatafanikiwa, yatatoa fursa ya kutumika kwa ratiba mpya ya safari katika reli ya Beijing hadi Shanghai kuanzia katikati ya mwezi Septemba.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako