• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sehemu ya kwanza ya Luteka ya pamoja ya majeshi ya majini ya China na Russia yamalizika

  (GMT+08:00) 2017-07-28 10:22:21

  Sehemu ya kwanza ya Luteka ya pamoja ya majeshi ya majini ya China na Russia imemalizika jana.

  Kundi la manowari la Jeshi la majini la China lilifunga safari mkoani Hainan, kusini mwa China tarehe 18 mwezi Juni na kuwasili bandari ya Baltiysk ya Russia tarehe 21 mwezi huu, na kushiriki kwenye luteka hiyo tarehe 25. Lengo la luteka hiyo ni kupata uzoefu wa kukabiliana na tishio la kigaidi baharini na kufanya mazoezi ya pamoja ya uokoaji, ambayo ni mara ya kwanza kufanyika katika bahari ya Baltic.

  Rais Vladimir Putin amesisitiza kwamba luteka hiyo kati ya Russia na China haimaanishi kuanzisha muungano mpya wa kijeshi, bali ni kuleta uwiano kwa dunia, na hailengi nchi yoyote. Amesema Russia na China zina ushirikiano wa kimkakati kwenye mambo ya kiuchumi, kisiasa na kijeshi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako