• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marufuku ya Joey Barton yapunguzwa

  (GMT+08:00) 2017-07-28 11:07:31

  kiungo wa zamani wa klabu ya Burnley Joey Barton amepunguziwa marufuku ya kutoshiriki masuala ya soka baada ya kukiuka maadili ya kuweka dau ya michezo (Betting) baada ya karibu miezi mitano baada ya kukata rufaa.

  Marufuku ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34 sasa itamalizika tarehe 1 Juni 2018, badala ya 25 October 2018. Alikuwa amepigwa marufuku mwezi Aprili baada ya kushtakiwa kwa kuvunja sheria za FA kwa kuweka dau (Bet) 1,260 kwa mechi kati ya Machi 26, 2006 na Mei 13 2016.

  Barton, ambaye amekiri kuwa yeye ni mraibu na mwenye mazoea ya kucheza kamari, alikata rufaa dhidi ya urefu wa marufuku ambayo alitaja kuwa ya "kupita kiasi".

  Bodi ya Rufaa ya FA ilisema marufuku ya awali ilikuwa ya "kupita kiasi katika hali" kwani ushahidi kutoka mshauri wa Barton ambaye ni mtaalamu wa saikolojia kuhusu madawa ya kulevya haikushirikishwa na wala haikufaa kukataliwa

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako