• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa mawaziri wa kazi na ajira wa BRICS wafungwa

    (GMT+08:00) 2017-07-28 16:59:19

    Mkutano wa mawaziri wa kazi na ajira wa nchi za BRICS wa mwaka 2017 umefungwa tarehe 27 mjini Chongqing, China, ambapo mawaziri wa kazi na ajira wa nchi za BRICS, wajumbe wa wenzi wa kijamii, pamoja na maofisa waandamizi wa Shirika la Kazi Duniani ILO na Shirikisho la Kimataifa la Utoaji wa Huduma za Kijamii, wamehudhuria mkutano huo na kufikia makubaliano mengi kuhusu masuala yanayofuatiliwa.

    Mkutano huo unafanyika kwa kufuata mipango ya mazungumzo ya viongozi wa nchi za BRICS, na kujadiliana kwa kina kuhusu masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na usimamizi wa dunia ya kazi katika siku za baadaye, uendelezaji wa uwezo wa kiufundi, utaratibu endelevu wa utoaji wa huduma za kijamii unaohusisha pande zote, na utekelezaji wa ahadi zilizotolewa katika mikutano iliyopita. Waziri wa raslimali watu na uhakikisho wa kijamii wa China Bw. Yin Weimin anasema:

    "Baada ya kufanya mjadala wa siku moja, tumepata ufahamu wazi zaidi kuhusu hali ya kazi kwa hivi sasa, hususan kwa fursa na changamoto zinazokabili soko la nguvu kazi katika nchi za BRICS, na kufikia makubaliano muhimu kuhusu namna ya kufanya ushirikiano na kutekeleza hatua kwa pamoja, ili kutoa ajira za kiwango cha juu zaidi na kazi zenye heshima, na kuhimiza uchumi wa dunia kupata ongezeko la kudumu."

    Ili kuimarisha ushirikiano kati ya nchi za BRICS katika sekta ya kazi na ajira, na kunufaisha zaidi watu wa nchi hizo, Bw. Yin Weimin ametoa mapendekezo matano: kuongeza nguvu kuhimiza utoaji wa ajira na kutimiza ongezeko shirikishi; kuhimiza mafunzo kuhusu uendelezaji wa uwezo wa kiufundi; kukuza ushirikiano katika utoaji wa huduma za kijamii; kuimarisha mawasiliano ya utamaduni katika sekta ya kazi na ajira na kuongeza nguvu katika ujenzi wa utaratibu.

    Mkutano huo unasisitiza kuwa, nchi mbalimbali zinatakiwa kuhimiza mfumo wa maendeleo ya uchumi na jamii unaosaidia utoaji wa ajira, kusukuma mbele uvumbuzi na uanzishaji wa biashara, ili kujenga utaratibu mwafaka na wenye ufanisi mkubwa zaidi wa usimamizi wa kazi, kuongeza ubora wa ajira na kuhimiza utoaji wa kazi zenye heshima. Mkutano huo umetangaza kuwa, ni lazima kuchukua hatua ili kuhimiza utimizaji wa malengo ya kuwasaidia watu maskini yaliyomo katika mipango ya maendeleo endelevu ya mwaka 2030, kuondoa na kupunguza umaskini kwa njia ya uendelezaji wa uwezo wa kiufundi, ili kuwasaidia watu kupewa fursa za kupata mafunzo ya kazi na kujifunza, na kuimarisha uratibu kati ya habari kuhusu soko la nguvu kazi na utoaji wa sera kuhusu uendelezaji wa uwezo wa kiufundi. Mkutano huo pia unaona kuwa utaratibu endelevu wa utoaji wa huduma za kijamii ambao unahusisha pande zote una umuhimu mkubwa katika kuhimiza ongezeko shirikishi, utoaji wa kazi za heshima na za uzalishaji, kutimiza uwiano wa kijinsia na muungano wa kijamii. Ingawa nchi wanachama wa BRICS zimepata maendeleo muhimu katika kuanzisha utaratibu kamili wa utoaji wa huduma za kijamii, lakini bado kuna pengo katika sekta za kuhusishwa na kiwango cha mshahara.

    Mkutano huo pia umepitisha Azimio la mwaka 2017 la Mkutano wa kazi na ajira wa nchi za BRICS, Waraka kuhusu msimamo wa pamoja wa usimamizi wa dunia ya kazi wa nchi za BRICS katika siku za baadaye, Mpango wa nchi za BRICS kuhusu kusaidia na kupunguza umaskini kwa kutumia uwezo wa kiufundi, Mfumo wa ushirikiano kuhusu utoaji wa huduma za kijamii wa nchi za BRICS, pamoja na Kanuni za mambo ya Mtandao wa Internet ya Mashirika ya utafiti kuhusu kazi za nchi za BRICS.

    Waziri wa raslimali watu na uhakikisho wa kijamii wa China Bw. Yin Weimin anasema:

    "Matokeo hayo yameonesha vya kutosha misimamo na ufuatiliaji wa pande mbalimbali, kuzingatia maoni tofauti na kuweka njia na hatua za kukabiliana na changamoto na matishio mbalimbali."

    Katibu mkuu wa Shirika la Kazi Duniani Bw. Guy Ryder akitoa hotuba katika mkutano huo alieleza kuwa, wakati uchumi wa dunia upo katika kipindi cha kupata mabadiliko na kutokuwa imara, kufanyika kwa mkutano huo wa mawaziri wa kazi na ajira wa nchi za BRICS kuna umuhimu mkubwa. Anasema:

    "Matokeo yaliyopatikana baada ya majadiliano ya pande mbalimbali katika sekta za usimamizi wa kazi katika siku za baadaye na kupunguza umaskini kwa kutumia uwezo wa kiufundi yana umuhimu mkubwa. Naona kuwa juhudi zenu pia zina umuhimu mkubwa katika kuhimiza kupeana uzoefu na kuinua kiwango cha kufanya ushirikiano kati ya nchi wanachama wa BRICS."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako