• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • TCRA yaondoa hofu kwa watumiaji wa mitandao ya simu

    (GMT+08:00) 2017-07-28 18:53:31

    Mamlaka ya mawasiliano Tanzania (TCRA) imewaondolea hofu watumiaji wa mitandao ya simu, wanaotaka kutumia huduma ya laini moja kwa mitandao yote, kuwa hatawakosa huduma zinazotolewa na makampuni ya simu.

    Kaimu naibu mkurugenzi wa maendeleo ya Tehama wa mamlaka Nehemia Mwenisongole, amesema huduma hiyo itakuwa ya hiari kwa watumiaji wa mitandao ya simu na itawasaidia kuondokana na kumiliki utitiri wa laini nyingi za simu na kutumia laini moja, iliyobeba mitandao yote ya simu ambayo atahitaji kutumia.

    Amewongeza kuwa iwapo mtu anaamua kuhamia kwenye mfumo huu wa kuunganishwa kutumia namba moja, hakutakuwepo na madhara ya kuanza kuwaza kuwa wapo watu ambao atawapoteza pindi anapoingia. Amesisitiza kuwa kuingia kwenye mfumo huo, kutasaidia kuondoa changamoto ya kukosekana kwa mtandao mahali mtumiaji atakapokuwa na kumsaidia kutumia mtandao mwingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako