• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Treni ya abiria Kenya yaongeza vituo vya kusimama wakati wa usafiri

    (GMT+08:00) 2017-07-28 18:53:49

    Treni ya abiria inayojulikana kama Madaraka Express sasa itaanza kusimama katika maeneo ya Voi na Mtito wa Andei kuanzia Agosti mwaka huu. Kampuni ya ya huduma za reli imesema hatua hiyo inalenga kuwawezesha abiria kushukia ama kupandia katika vituo hivyo.Akizungumza na na radio China Kimataifa, Mkurugenzi mkuu wa shirika hilo Bwana Atanas Maina amesema huduma hiyo itawawezesha abiria kukata tiketi zao kutoka mjini Nairobi ama Mombasa hadi katika vituo hivyo viwili. Ameongeza kuwa idadi ya abiria imeongezeka tangu huduma hiyo ianzishwe mei mwaka huu.Amesema kuwa awali treni ya abiria ilikuwa ikisafirisha watu 1,400 kila siku lakini idadi hiyo imeongezeka na kufikia 2,700 kwa siku.Ametaja hatua hiyo kuwa afueni kwa abiria.Aidha Bwana Maina amesema huduma za kusimama katika vituo vya Mariakani, Miasenyi, Kibwezi, Emali na Athi River zitaanza pindi treni ya kuhudumia kaunti mbali mbali litakapoanza shughuli zake.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako