• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Magufuli aitikia ombi la wafanyabiashara kwenye kituo cha Msavu

    (GMT+08:00) 2017-07-28 18:54:10

    Rais John Pombe Magufuli ameitikia ombi la wafanyabiashara wadogowadogo kwa kuwaruhusu kuendelea kufanya biashara kwenye kituo kikuu cha mabasi cha Msamvu.

    Wafanya biashara hao wamelalamikia kunyanyaswa na viongozi wa Manispaa ya Morogoro wakisema wamekuwa wakifukuzwa wasifanye biashara tangu kituo cha mabasi cha Msamvu kijengwe upya.

    Rais Magufuli pia amemuagiza kamanda wa polisi wa Mkoa, Ulrich Matei kuhakikisha kwamba askari mgambo hawawasumbui tena wafanyabiashara hao.

    Pamoja na kumuagiza Kamanda Matei kuchukua hatua hiyo, Rais pia aliwataka wafanyabiashara hao kutofanya vurugu wakati utaratibu mzuri wa kufanya biashara katika eneo hilo unaandaliwa kwa ajili yao. Aidha, rais Magufuli pia amewataka watu wote walioshindwa kuviendeleza viwanda vilivyobinafsishwa kwao, kuvirejesha serikalini ili wapewe wawekezaji wenye uwezo wa kuviendeleza na kuzalisha ajira.

    Kuhusu kilimo, Magufuli amewapongeza wakulima wa mazao mkoani Morogoro kwa kuongeza uzalishaji wa mazao na hasa wakulima wa Kilosa, ambao amesema wameongeza uzalishaji kutoka asilimia 42 kwa msimu wa kilimo uliopita hadi kufikia asilimia 82 msimu huu

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako