• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiwango cha watu wasiokuwa na ajira chapungua nchini China

    (GMT+08:00) 2017-07-28 19:33:46

    Takwimu rasmi zinaonesha kuwa kiwango cha watu wasiokuwa na ajira katika miji ya China kipo kwenye asilimia 3.95 hadi kufikia mwishoni mwa robo ya pili ya mwaka, ambapo kimefikia kiwango cha chini zaidi katika miaka ya karibuni.

    Wizara ya Rasilimali Watu na Usalama wa Kijamii MHRSS imetangaza kuwa kiwango hicho kimeshuka kidogo kikilinganishwa na asilimia 3.97 ya robo ya kwanza, na pia kikiwa chini kikilinganishwa na kile cha asilimia 4.05 cha mwaka jana wakati kama huu. Aidha imesema China imetoa ajira milioni 7.35 katika nusu ya kwanza ya mwaka, ambazo ni laki 1.8 zaidi kuliko mwaka jana wakati kama huu.

    Katika mkutano na wanahabari afisa mwandamizi wa MHRSS amesema soko la ajira linaendelea kuwa tulivu na limekuwa msingi wa wa maendeleo ya uchumi na utulivu wa jamii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako