• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaihimiza Korea Kaskazini ifuate azimio husika la Baraza la Usalama

    (GMT+08:00) 2017-07-29 15:40:20

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo amesema, China imeihimiza Korea Kaskazini ifuate azimio husika la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na kusitisha shughuli zozote zinazowezekana kuzidisha wasiwasi wa hali ya peninsula ya Korea.

    Bw. Geng Shuang amesema China inafuatilia maendeleo ya tukio hilo. Na China inapinga Korea Kaskazini kukiuka azimio la Baraza la Usalama na matumaini ya jumuiya ya kimataifa, na kurusha makombora.

    Bw. Geng Shuang pia amesema China inazitaka pande mbalimbali zichukue hatua kwa umakini, kuzuia hali kuwa mbaya zaidi, na kulinda kwa pamoja amani na utulivu wa kikanda.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako