• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atoa agizo la jeshi la China kuongeza uwezo wa mapambano

    (GMT+08:00) 2017-07-30 13:39:03

    Rais Xi Jinping ametoa agizo akitaka jeshi la China kuongeza uwezo wa mapambano na kuimarisha ulinzi wa kisasa wa taifa.

    Rais Xi ambaye pia ni katibu mkuu wa chama tawala nchini China, Chama cha kikomunisti, na mwenyekiti wa kamati ya kijeshi ya chama, ametoa agizo hilo leo asubuhi baada ya kukagua gwaride la kijeshi lililofanyika katika kituo cha kijeshi cha Zhurihe, kaskazini mwa China. Gwaride hilo ni sehemu ya pilkapilka mbalimbali katika maadhimisho ya miaka 90 ya kuanzishwa kwa jeshi la ukombozi la umma la China, ambayo itakuwa tarehe 1 Agosti.

    Rais Xi alisema, jeshi la ukombozi la umma la China ni lazima lichukulie uwezo wa mapambano kama kiwango pekee cha kimsingi, kujizatiti kwa vita, na kujenga jeshi imara ambalo siku zote liko tayari kwa vita, kuwa na uwezo wa mapambano na kwa hakika linapata ushindi.

    Vile vile alitaka maaifsa na askari kujenga jeshi lenye ufahamu wa kisiasa, kuimarisha jeshi kwa kufanya mageuzi, kuendeleza jeshi kwa sayansi na teknolojia, na kusimamia jeshi kwa mujibu wa sheria, ili kuinua kiwango cha ulinzi wa kisasa taifa na jeshi la kisasa.

     

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako