• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gwaride la kijeshi la China laonyesha mafanikio ya mageuzi ya kijeshi

    (GMT+08:00) 2017-07-31 10:24:42

    Kamanda mkuu wa gwaride ya jeshi la China Bw Han Weiguo amesema, gwaride la maadhimisho ya miaka 90 ya kuanzishwa kwa jeshi la ukombozi la umma la China PLA limeonyesha mafanikio ya mageuzi ya kijeshi ya China.

    Amesema gwaride hilo limeonyesha mfumo mpya, muundo mpya na mafanikio mapya tangu jeshi la China lianze mageuzi, kuonyesha wazo jipya, muundo mpya na uwezo mpya wa kujenga jeshi lenye kiwango cha juu duniani. Pia limewaonyesha wananchi wote wa China kuwa, jeshi la China litalinda umoja wa kitaifa na ukamilifu wa ardhi, na ni nguvu imara ya kulinda amani ya dunia.

    Habari nyingine zinasema, kikosi cha kulinda amani cha China nchini Sudan Kusini, jana huko Wau kilifanya maadhimisho ya miaka 90 ya jeshi la ukombozi la umma la China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako