• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Micho hatimaye akigura Uganda Cranes

    (GMT+08:00) 2017-07-31 10:39:03

    Mkufunzi mkuu wa timu ya soka ya Uganda, Uganda Cranes Micho Sredojevic amesitisha mkataba wake na shirikisho la kandanda la nchi hiyo FUFA akilalamikia kutolipwa mshahara na marupurupu ya shilling million 230 pesa za Uganda.

    Akizungumza na wanahabari, Micho alifichua kuwa mkataba wake na Cranes ulisitishwa kwani alikosa kuafikiana na FUFA kuhusiana na jinsi suala hilo lingeshughulikiwa. Micho alisisitiza kuwa alifanya majukumu yake kama kocha wa Cranes kwa uhaminifu na hakuelewa ni kwa nini FUFA ilipata ugumu kumpa haki yake.

    Raia huyo wa Serbia hata hivyo amewashukuru wachezaji wa timu ya taifa ya soka ya Uganda kwa uadilifu wao wakati amekuwa kocha wao. Alikiri kuwa uamuzi huo ulikuwa mgumu lakini akasema atabaki shabiki wa timu hiyo japo ameigura.

    Mchakato wa kutafuta kocha atakayejaza nafasi yake umeanza huku makocha wa zamani wa Kenya Adel Amrouche na Luc Eymael wakipewa upato kuteuiliwa kwa wadhifa huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako