• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wanariadha wa Kenya wawaonya wapinzani wao

    (GMT+08:00) 2017-07-31 10:39:43

    Bingwa wa dunia wa mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji Hyvin Kiyeng na wanariadha wenzake kutoka Kenya wameahidi kushiriki mashindano ya dunia yatakayofanyika jijini London kwa ushirikiano mkubwa ili kuwanyamazisha wapinzani wao wakuu Katika mbio hizo.

    Kiyeng ataungana na bingwa wa mbio za mita 3000 kuruka viunzi na maji katika kitengo cha chipukizi wasiozidi miaka 20 Cellphine Chespol, na mshindi wa mbio za jumuia ya madola Purity Kirui na Beatrice Chepkoech katika mashindano ya London, na wanne wao wameahidi kuweka kando ndoto zao za kibinafsi na kuhakikisha mmoja wao ameshinda taji hilo.

    Aidha kiyeng amewaonya wapinzani wao, hasa mwanariadha aliyezaliwa Kenya Ruth Chebet anayekimbilia taifa la Bahrain kwa sasa, ambaye pia ni Bingwa wa Olimpiki na mwenye kushikilia rekodi ya dunia, kwamba awe tayari kwa kiputwe kikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako